Home Uncategorized KAGERE, MSUDAN NDANI YA NYUMBA SIMBA

KAGERE, MSUDAN NDANI YA NYUMBA SIMBA


Wachezaji wa kimataifa wa Simba, akiwemo Meddie Kagere na Sharaf Shiboub wanaanza kuwasili jijini Dar es Salaam, kesho ijumaa tayari kujiandaa na msimu mpya wa ligi simba  inaondoka wikiendi hii kwenda kambini nchini Afrika Kusini kwa ajili ya msimu mpya wa Ligi Kuu Bara katika kambi itakayoanza Jumatatu ijayo.

Kikosi cha simba kilichosajiliwa msimu huu ni pamoja na Kagere, Shiboub, Francis Kahata, Tairone santos da silva, Person Fraga Viera, Wilker Henrique da silva, Deo Kanda, Ibrahim Ajibu, Beno Kakolanya na Kennedy Juma.

Wachezaji wengine ni John Bocco, Pascal Wawa, shomari Kapombe, Erasto Nyoni, Aishi Manula, Clatous Chama, Jonas Mkude, Rashid Juma, Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ Hassan Dilunga, said Ndemla na Mzamiru Yassin.

Katibu Mkuu wa simba, Arnold Kashembe amesema; “Wachezaji wote wa kimataifa wanatarajia kuanza kuwasili jijini siku ya Ijumaa na baada ya hapo ndio maandalizi ya kambi yataendelea ambayo itaanza Julai 15.

“Kocha Patrick Aussems akiwasili mapema atajiunga na kikosi kwa ajili ya kambi na kama akichelewa basi kocha msaidizi ataanza kukinoa kikosi.”

Ofisa Habari za simba, Haji Manara alisema kuwa timu hiyo itaondoka Dar es salaam wikiendi hii na kufika Jumatatu hawatakuwepo Dar bila kufafanua itakuwa wapi.

“Kufikia Jumapili hatutakuwepo Dar es salaam tutakwenda kambini,” alisema Manara na kuongeza: “Huu usajili tuliofanya wa wachezaji Kakolanya (Beno), Gadiel (Michael) na Ajibu (Ibrahim) ni kama tumewapiga hat trick Yanga kwa kuwachukua wachezaji wao hawa watatu.”

SOMA NA HII  MUONEKANO WA UKURASA WA NYUMA GAZETI LA CHAMPIONI IJUMAA