Home Uncategorized MANCHESTER CITY: HATUJAPATA OFA YA BAYERN MUNICH KUMTAKA SANE

MANCHESTER CITY: HATUJAPATA OFA YA BAYERN MUNICH KUMTAKA SANE


PEP Guardiola, Meneja wa Manchester City amesema kuwa hajapata ofa yoyote kutoka kwa Bayern Munich ikimhitaji mchezaji wao Leroy Sane.

Munich imeelezwa kuwa inahitaji saini ya winga huyo kwa ajili ya msimu ujao.

“Bado sijapata taarifa yoyote kutoka kwa Bayern Munich wakihitaji saini ya Sane kama itatokea ni jambo la kuzungumza.

“kwa sasa ninachoangalia ni maendeleo ya kikosi changu kwa ajili ya msimu ujao na ninafurahi kuona kila mchezaji ana furaha,” amesema.

SOMA NA HII  HESABU ZA KAGERA SUGAR KWA YANGA BADO KABISA