Home Habari za Simba Leo MO DEWJI AONESHA JEURI YA PESA…BIL 6 KUFANYA USAJILI TU

MO DEWJI AONESHA JEURI YA PESA…BIL 6 KUFANYA USAJILI TU

habari za simba, mo dewji simba

KWELI TAJIRI KAVUNJA BENKI, Unaweza kusema kivyo baada ya Muwekezaji na Raisi wa Heshima wa Simba Mohamed Dewji kuiwezesha SIMBA, kufanya fujo ya usajili hapa Afrika.

Simba inaelezwa kuwa imetumia zaidi ya BILLION 6 za Kitanzania kwenye dirisha la usajili 2024/25 ikiwemo gharama zote za Wachezaji wapya, nyongeza ya mikataba ya Wachezaji wa zamani (Extension) na gharama za benchi la Ufundi pamoja na gharama za kuwalipa Scouts barani Afrika na nje ya Afrika.

Hadi sasa Simba imefanya usajili wa wachezaji wa Kimataifa pekee wapya, 11 huku wakibakiza nafasi moja kumamilisha idadi inayohitajka ya wachezaji wa kigeni.

Simba imewasajili kwa dau kubwa zaidi msimu huu wachezaji wafuatao, Joshua Mutale, Jean Charles Ahoua, Steve Mukwala, Augustine Okejepha, Chamou Karaboue, Deborah Ferndandes, Valentine Nouma.

Wachezaji wa zamani ni Ayub Lakred aliyeongeza mkataba, Che Fondoh Malone, Fabrice Ngoma, na Freddy Michael Kaublan.

Msimu uliopita Mwekezaji MO Dewji alitumia BILLION 3 ila msimu huu imeenda zaidi ya mara mbili ya msimu uliyopita hivyo amezidisha mara mbili.

Taarifa zinaeleza kwamba Simba itaachana na wachezaji wengine kwa kuwavunjia mikataba na ivyo wanapaswa kulipa fidia.

Hadi sasa Simba imeachana na wachezaji wakubwa kadhaa ikiwemo Clatous Chama ambaye mazungumzo ya kumuongeza mkataba mpya hayakufanikiwa, na akajiunga na Ynaga, Saidoo Ntibazonkiza, Henock Inonga aliyeuzwa, Luis Miquissone John Bocco na Kennedy Juma.

Huku majina mengine kama Babacar SAR, Sadio Kanoute, Par Omar Jobe, Willy Esomba Onana, Aubin Kramo yakiwekwa kwenye mabano muda wowote yatatanazwa kuachwa.

SOMA NA HII  UKICHEZA NA SIMBA HII....JIANDAE KWA LOLOTE AISEE...KAMA SI NYEKUNDU BASI NJANO INAKUHUSU...