Home Habari za Simba Leo BARUA YA WAZI..AHMED ALLY APEWE MAUA YAKE…SIMBA HAIJAKOSEA KUMSAJILI

BARUA YA WAZI..AHMED ALLY APEWE MAUA YAKE…SIMBA HAIJAKOSEA KUMSAJILI

Habari za Simba SC

Jina lake ni Ahmed Ally, A.K.A Mashine ya Kuongea au Semaji la CAF, Msemaji aliyepitia kipindi kigumu Lakini aliendelea kuisimamisha CHAPA/Brand ya Simba kileleni kunakostahili.

Huyu Mwamba hata akililala anaiwaza Simba, akipumua anaiwaza namna Gani kuisemea Simba Ili aeleweke kwa mashabiki.

Hebu itazame SIMBA kwa Miaka mitatu hii Mfululilizo kisha mtazame Ahmed Ally na Kispika chache mithiri ya Machinga muuza Urembo au muuza dawa za Kunguni. Alihakikisha anapita mtaa kwa mtaa kuhakikisha Wanasimba hawawi wanyonge.

Aliwaambia Wanasimba nyie ndiye wenye Inchi mnapaswa kutembea kifua mbele.Nyuma yake Wanasimba walimfata kwa Shangwe na Vigelele huku akiwashawishi Maneno matamu ili Hali Timu ikiwa Katika wakati mgumu.

Pengine Maneno yake yaligeuza Shubiri na kuwa Sukari midomoni mwa Wanasimba….

Ahmed Ally alikuwakumbusha Wanasimba kuwa Duniani kuna Simba Mmoja tu Wakariakoo, pamoja na SIMBA kupitia manyangaso, Mateso Raha na karahaa, Umaskini na Utajiri lakini Ahmed Ally aliendelea kuwafanya wanasimba kuwa na Imani kubwa kwa Club yao.

Pamoja na Uongozi wa Club kutokuwa imara kwenye kumshughulikia matatizo ya Ndani, Ahmed Ally aliendelea kuibeba Timu mabegani..Ilipo Simba yeye aliibeba na kuisemea, Mkoani Hadi Vijijini Alifika.

Pamoja na Matawi ya Club kutengwa Bado Ahmed lipita kwenye Matawi Pale kwa Wekundu wa Terminal Dar Es Salaam hadi Hadi Simba Burudani Arusha alifika Nyakato hadi kibondo kwa Bibi hakusahau Ahmed Ally alisimama Imara kuitetea Nembo ya Club

Ukimchukia Ahmed Ally umeuchukia Mpira ,hivi ni Kipi Ahmed Ally Hajafanya?

Ahmed Ally alikuja Simba katika mda muafaka kwani Hakuna Afisa wa Habari ambaye angefanya kazi katika taasisi ambayo ilipita Kipindi kigumu..

Mbali na Simba kufanya vibaya bado Simba iliendelea kuzumgumzwa Mitandaoni hadi kwenye vyombo vya Habari. Brand Ya Simba inaendelea kusimama imara.

PENGINE Msimu ujao Simba ikifanya vizuri Kuna watu wanafunga akaunti zao, redio hadi Tv Jeshi La Mtu mmoja ambalo linapambana na majeshi Zaidi ya Manne Katika mpira wa Tanzania na Bado kashikilia usukani anasonga Mbele Hakuna wakumzuia, Simba hii Mbovu na Bado hajazuilika Sasa Vuta picha Simba Imara kuna watu wanarusha Ngumi.

Ahmed Ally ameipenda Simba anaitumikia Simba Zaidi ya makubalino ya mkataba wa Kazi. Semaji CAF linazungumza watu hutega masikio pengine ndiyo makosa makubwa wanayofanya .

Ukimchukia Ahmed basi umeuchukia Mpira wa Tanzania.

SOMA NA HII  YANGA YAZIPIKU SIMBA, AZAM FC UPIGAJI MASHUTI...YASUBIRI TUZO ZA TFF