Home Uncategorized WABRAZIL SIMBA WAPIGA TIZI LA SAA MBILI DAR

WABRAZIL SIMBA WAPIGA TIZI LA SAA MBILI DAR


WACHEZAJI watatu raia wa Brazil waliosajiliwa na Simba hivi karibuni, tayari wameanza mazoezi jijini Dar huku kikosi kamili cha Simba kikiwa bado hakijaanza mazoezi.

Wachezaji hao ni mshambuliaji Wilker Henrique da Silva, kiungo mkabaji, Gerson Fraga Vieira na beki, Tairone Santos da Silva, wamejiunga na Simba hivi karibuni na watatumika kwenye msimu ujao ambao Simba itashiriki mashindano mbalimbali ikiwemo Ligi Kuu Bara wakiwa mabingwa watetezi na Ligi ya Mabingwa Afrika.

Simba imewasajili wachezaji hao kila mmoja kwa mkataba wa miaka miwili. Championi linafahamu wachezaji hao wameanza mazoezi katika Hoteli ya Sea Scape ambayo inatumiwa na timu hiyo kuweka kambi wakati wote.

Chanzo cha kuaminika kimeliambia Championi Jumatano kuwa wachezaji hao wameanza mazoezi hayo tangu Jumatano ya wiki iliyopita baada ya kuhamishiwa kwenye hoteli hiyo kutoka katika hoteli ya Sea Cliff.

“Wale wachezaji wa Brazil ambao wameshasaini mikataba wanafanya mazoezi ya Gym jioni pale hotelini, asubuhi wanakuwa wanakwenda ufukweni kukimbia kwa zaidi ya saa mbili kabla ya kurejea lakini walikwenda Uwanja wa Taifa siku chache nyuma,” kilisema chanzo.

Alipotafutwa katibu wa timu hiyo, Dk Arnold Kashembe alikiri kuwa wachezaji hao wanafanya mazoezi hayo kwa kuwa hawatarajii kurejea nchini kwao kutokana na muda kubakia mdogo kabla ya kuanza maandalizi ya msimu mpya.

CHANZO: CHAMPIONI

SOMA NA HII  KIKOSI CHA YANGA KITAKACHOANZA LEO DHIDI YA POLISI TANZANIA