Home Uncategorized HAWA NDIO UD SONGO WAPINZANI WA SIMBA KIMATAIFA, UKIWAPIGA MAPEMA WANAPOTEANA MAZIMA

HAWA NDIO UD SONGO WAPINZANI WA SIMBA KIMATAIFA, UKIWAPIGA MAPEMA WANAPOTEANA MAZIMA


 UD Songo ya Msumbiji msimu uliopita walishiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa na kutupwa nje na Nkana FC ya Zambia ambayo nayo ilipigwa chini na Simba.

Sasa leo wapo kazini kwenye mchezo wa awali dhidi ya Simba utakaochezwa nchini Msumbiji. 

Kwenye mechi 14 za ligi ambazo wamecheza wameshinda jumla ya mechi 8 wamelazimisha sare mechi mbili na kupoteza mechi 4.

UD Songo ni timu inayofanya counter attack nyingi na wana kasi ya hali ya juu. Hivyo Simba leo lazima kuwa makini kuwadhibiti kwa kuwawahi mapema.

Hata hivyo msimu uliopita haikuwa hatari katika umaliziaji kwa kuwa ilikosa washambulizi bora na wazoefu.

Msimu huu kikosi hicho kimefanya marekebisho kadhaa wakiwa na nia ya kufika mbali kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika karata yao ya kwanza ni leo mbele ya Simba wakiwa nyumbani kwao.

SOMA NA HII  YANGA WASHINDWA KUTAMBA UGENINI, WAPOKEA KIPIGO KIZITO