Home Uncategorized KOCHA STARS: WACHEZAJI SASA WAMEANZA KUIVA, TIMU KUTIA TIMU BONGO LEO

KOCHA STARS: WACHEZAJI SASA WAMEANZA KUIVA, TIMU KUTIA TIMU BONGO LEO

SELEMAN Matola, Kocha msaidizi wa timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ amesema wachezaji wameanza kucheza soka linaloeleweka wakiwa uwanjani tofauti na mwanzo jambo linalotoa picha kwamba mchezo wa marudio watafanya vema.

Jana Stars ililazimisha sare ya kufungana bao 1-1 na timu ya Taifa ya Burundi kwenye mchezo wa kwanza wa kufuzu Kombe la Dunia nchini Qatar mwaka 2022.

Matola amesema: “Kuna makosa madogomadogo ambayo yanafanywa na wachezaji ambayo yakifanyiwa kazi yataleta matokeo chanya na bora kwa kila mchezaji


 “Kazi kubwa tunapaswa tuifanye nyumbani tukiwa uwanja wa Taifa kutafuta matokeo chanya, ni muda wa mashabiki kuendelea kutoa sapoti ya kutosha ili kuongeza hamasa,” amesema.

Stars inatarajiwa kutia timu leo majira ya saa kumi na moja jioni ikitoa nchini Burundi kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa marudio dhidi ya Burundi utakaopigwa Septemba nane, uwanja wa Taifa.

SOMA NA HII  KASI YA AZAM FC YAIPA PRESHA SIMBA