Home Uncategorized MAYWEATHER KUPAMBANA TENA NA MCGREGOR NA KHABIB

MAYWEATHER KUPAMBANA TENA NA MCGREGOR NA KHABIB


BONDIA Floyd Mayweather ameibuka na kuthibitisha kwamba atapambana na Conor McGregor na Khabib Nurmagomedov katika pambano la kurejeana mwaka huu.

Nguli huyo wa ndondi kutoka Marekani alimshinda M-Ireland huyo huko Las Vegas Agosti 2017 katika pambano la raundi 10.

Lakini kumekuwa na kelele kutoka kwa mashabiki wakitaka kuona pambano jingine la Mayweather,  na bondia huyo amewasuuza moyo mashabiki wake baada ya kutoa tangazo hilo kwenye Instagram muda mfupi tu baada ya McGrgeor kurejea tena ulingoni na kupata ushindi wa kishindo wa TKO kwa kumtwanga mpinzani wake, Donald ‘Cowboy’ Cerrone, kwa sekunde 40 tu.

Bosi wa UFC, Dana White, amethibitisha kuwepo ka pambano hilo kwani mazungumzo yameshaanza ambapo mwanzoni mwa wiki hii McGregor aliongea kuhusu azma yake ya kupambana tena na Mayweather.
SOMA NA HII  MSHAMBULIAJI ALIYEKUWA ANAWINDWA NA YANGA AIBUKIA POLISI TANZANIA