Home Uncategorized AZAM FC: TUPO TAYARI KUPAMBANA NA NAMUNGO

AZAM FC: TUPO TAYARI KUPAMBANA NA NAMUNGO

UONGOZI wa Azam FC umesema kuwa upo tayari kupambana na Namungo leo kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaochezwa Uwanja wa Majaliwa.

Azam FC inakumbukumbu ya kulazimisha sare ya kufungana bao 1-1 na Ndanda kwenye mchezo uliopita uliochezwa Uwanja wa Nangwanda Sijaona.

Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Azam FC, Jafary Maganga amesema:-“Kila kitu kipo sawa tunatambua mchezo utakuwa mgumu ila mwalimu amewapa mbinu wachezaji ambazo zitawapa ushindi ndani ya uwanja.

“Wapinzani wetu tunawaheshimu kwani wamekuwa kwenye ushindani mkubwa nasi tutapambana kupata matokeo mashabiki watupe sapoti,”.

SOMA NA HII  MAXI NZEGELI KWA YANGA SASA HIVI NI ZAIDI YA SHUJAA