Home Uncategorized HAWA HAPA WATAJWA KUWA KISIKI CHA MPINGO KWA LIVERPOOL EPL

HAWA HAPA WATAJWA KUWA KISIKI CHA MPINGO KWA LIVERPOOL EPL

MECHI ya Ligi Kuu England kati ya Norwich dhidi ya Liverpool inatajwa kuwa kikwazo kwa timu ya Liverpool ambayo haijapoteza mchezo hata mmoja msimu huu.

Liverpool inaongoza ligi ikiwa na pointi 73 baada ya kucheza mechi 25, imeshinda 24 na sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Manchester United.

Februari 15, inatarajia kumenyana na Norwich jambo ambalo linaipa ugumu Liverpool ya Jurgen Klopp kutokana na mwenedo wa wapinzani wao na wanatajwa kuwa watakuwa kisiki cha mpingo.

Kwenye mchezo wa kwanza, Liverpool ikiwa Anfield waliibuka na ushindi wa mabao 4-1 ila kwa sasa watakuwa ugenini.

Inatajwa kuwa mechi ngumu kutokana na ukweli kwamba Norwich inapambana isishuke daraja ipo nafasi 20.

Ni vita ya kinara wa ligi na yule anayeshika mkia akiwa na pointi 18 baada ya kucheza mechi 25 imeshinda mechi nne pekee, sare sita na kupoteza 15.

Licha ya kuonekana wabovu pale kwenye uwanja wao wa nyumbani Carrow Road huwa wanakuwa na moto Manchester City ilichapwa mabao 3-2 lolote linaweza kutokea.

SOMA NA HII  SVEN KOCHA MKUU WA SIMBA ATWAA TUZO YA KOCHA BORA WA VPL