Home Uncategorized MABOSI WA YANGA WAPANIA KUWA NA KIKOSI MATATA AFRIKA MASHARIKI NA KATI

MABOSI WA YANGA WAPANIA KUWA NA KIKOSI MATATA AFRIKA MASHARIKI NA KATI

UONGOZI wa Yanga umesema kuwa mpango mkubwa wa kuboresha kikosi chao kwa sasa ni mkubwa na wana imani ya kuwa na kikosi bora mwakani.

Kwa sasa Yanga ipo kwenye mchakato wa kuboresha kikosi chini ya wanafamilia ya GSM ambao wapo nao bega kwa bega katika masuala ya usajili na uwekezaji.

Mkurugenzi wa Uwekezaji na Uendeshaji ndani ya GSM, Injinia Hersi Said kupitia kwa Ofisa Uhamasishaji wa Yanga Antonio Nugaz amesema:”Tuendelee kuijenga timu yetu ya Yanga kwa maendeleo ya kweli ila mwakani Insha Allah weka akilini mwako kuwa tutakuwa na kikosi imara zaidi kuliko timu yeyote kwenye ligi yetu na hata Afrika Mashariki na kati,”.

Miongoni mwa wachezaji ambao wanatajwa kupewa dili ndani ya Yanga ni pamoja na nyota wa timu ya Namungo Lusajo Relliants, Bigirimana Blaise, Ayoub Lyanga. Sure Boy na Marcel Kaheza kwa wachezaji wa ndani huku Mussa Mohamed wa Nkana FC akitajwa kuwindwa na Yanga.

SOMA NA HII  TFF YAIJIBU SERIKALI KUHUSIANA NA KUGOMEA VIKAO VYAKE