Home Uncategorized MBICHWA WA SAMATTA WAFANYA YAKE KWA MARA YA KWANZA NDANI YA EPL,...

MBICHWA WA SAMATTA WAFANYA YAKE KWA MARA YA KWANZA NDANI YA EPL, LICHA YA TIMU YAKE KUPOTEZA



MBWANA Samatta, nahodha wa timu ya Taifa ya Tanzania ameweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kutoka ardhi ya Bongo kufunga bao ndani ya Ligi Kuu England.

Samatta anayekipiga ndani ya Klabu ya Aston Villa, amefunga bao lake la kwanza ndani ya ligi hiyo kwenye mchezo wake wa kwanza wa ligi baada ya kujiunga na Villa kwa kandarasi ya miaka minne na nusu akitokea Genk ya Ubelgiji .

Bao pekee la Samatta na la kufutia machozi kwa Villa lilipachikwa dakika ya 70 ya kipindi cha pili kwa kichwa na wakati ikifungwa mabao 2-1 na Bournemouth.

Mabao ya Bournemouth yalifungwa na Philip Biling dk 37 na Nathan Ake dk ya 44, timu hiyo ilimaliza ikiwa pungufu baada ya Jefferson Lerma kuonyeshwa kadi nyekundu dk ya 51.

Aston Villa inashuka mpaka nafasi ya 17 ikiwa na pointi 25 baada ya kucheza mechi 25 na Bournemouth ipo nafasi ya 16 ikiwa na pointi 26.

SOMA NA HII  MUANGOLA WA YANGA HATIHATI KUKOSA MECHI ZOTE ZA MZUNGUKO WA KWANZA