Home Uncategorized RAHEEM STERLING ATAKA CHANGAMOTO MPYA

RAHEEM STERLING ATAKA CHANGAMOTO MPYA

RAHEEM Sterling, nyota wa Manchester City iliyo chini ya Pep Guardiola amesema kuwa hana mashaka iwapo atahitaji kuondoka ndani ya Klabu hiyo kwani naye anahitaji kupata changamoto mpya.
Sterling ameyasema hayo alipokuwa akihojiwa na gazeti moja la Spanish kuhusu maisha yake ndani ya City na kama anaweza kutimka hapo na kujiunga na Real Madrid ambao inaelezwa wanahitaji saini yake.
“Wakati wangu ujao ni mzuri kuutazama, ila ni matumaini ambayo yapo ama kuna mtu ambaye anatambua kuhusu hilo? 
“Muda wote nahitaji changamoto mpya na ila kwa sasa changamoto zangu mpya kwa sasa ni ndani ya City ambayo nipo muda huu ila haya mambo yanayoendelea inaweza kuwa iwapo kuna mipango ambayo itapangwa kwani hakuna kinachotokea bila kupangwa,” amesema.

SOMA NA HII  KUSAJILI WAPYA SAWA, LAKINI KWA JAMES KOTEI MTAKOSEA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here