Home Uncategorized SABABU ILIYOWAPONZA WACHEZAJI WA YANGA KUSHINDWA KULINDA USHINDI KWA POLISI TANZANIA

SABABU ILIYOWAPONZA WACHEZAJI WA YANGA KUSHINDWA KULINDA USHINDI KWA POLISI TANZANIA

NAHODHA wa Yanga, Papy Tshishimbi amesema kuwa kilichowaponza kushindwa kupata ushindi mbele ya Polisi Tanzania Uwanja wa Ushirika ni ubovu wa Uwanja huo.

Tshishimbi aliongoza kikosi chake kuambulia pointi moja mbele ya Polisi Tanzania kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara jana, Februari 18.

“Tulipata bao la kuongoza na tulifurahi mwisho wa siku takashindwa kulinda bao letu kutokana na ugumu wa eneo la kuchezea kwani mpira ulikuwa hautulii na mwisho wa siku wenzetu wakatushinda.

“Wao walikuwa ni wenyeji na wanautambua vizuri uwanja wakatumia nafasi hiyo kushinda, tunashukuru kwa kuwa tumemaliza salama mchezo ni mwendelezo wetu kujipanga kwa jili ya mechi zinazofuata.” amesema.
SOMA NA HII  SIMBA NA YAHYA MBEGU MPAKA KIELEWEKE