Home Uncategorized KOCHA NAMUNGO AWAPA PROGRAMU MAALUMU WACHEZAJI WAKE

KOCHA NAMUNGO AWAPA PROGRAMU MAALUMU WACHEZAJI WAKE


HITIMANA Thiery, Kocha Mkuu wa Namungo amesema kuwa amewapa programu wachezaji wake wakati huu wa mapumziko ili kuona wanalinda vipaji vyao.

Namungo ya Ruangwa inashiriki Ligi Kuu Bara kwenye msimamo ipo nafasi ya nne ikiwa imejikusanyia pointi 50 baada ya kucheza mechi 28.

Kwa sasa ligi imesimama kwa muda ili kuzuia maambukizi ya Virusi vya Corona na inatarajiwa kurejea iwapo hali itakuwa shwari.

Akizungumza na Saleh Jembe, Thiery amesema kuwa anatambua kwamba wachezaji wake watapata muda wa kupumzika jambo lililowafanya awape programu wachezaji wake.

“Nimewapa programu maalumu wachezaji wangu nina amini itawafanya wawe bora na tutakaporejea kwenye ligi nina amini tutaendelea palepale ambapo tuliishia kikubwa ni wachezaji wangu kujilinda na kutimiza maelekezo.

“Pia nimewaambia kwamba wasisahau kujilinda na kuchukua tahadhari kwa ajili ya Virusi vya Corona kwani hili ni janga la Taifa,” amesema.

SOMA NA HII  MASHABIKI WA SIMBA KUPIGA PICHA BURE NA KOMBE NI HASARA