Home Uncategorized MBAO KWENYE MTIHANI MBELE YA YANGA LEO TAIFA

MBAO KWENYE MTIHANI MBELE YA YANGA LEO TAIFA

MBAO iliyo chini ya Kocha Mkuu, Abdulmutik Hajji leo ina kazi nzito mbele ya Yanga kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaochezwa Uwanja wa Taifa.

Mchezo wa leo utachezwa majira ya saa 1:00 usiku Uwanja wa Taifa unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kwa timu zote mbili.

Mbao FC imekuwa kwenye mwendo wa kusuasua ikiwa imetoka kupoteza mbele ya Ruvu Shooting kwa kuchapwa mabao 2-0 huku Yanga ikiwa imetoka kuichapa Alliance mabao 2-0 Uwanja wa Taifa.

Mbao ipo nafasi ya 15 kibindoni ina pointi 22 ikiwa imecheza mechi 25 huku Yanga ikiwa nafasi ya nne na ina pointi 44 ikiwa imecheza mechi 23.

SOMA NA HII  YANGA: TUNAIFUNGA SIMBA MACHI 8 MAPEMA TU