Home Uncategorized VITA YAO LEO MANCHESTER UNITED V MANCHESTER CITY

VITA YAO LEO MANCHESTER UNITED V MANCHESTER CITY


LEO Uwanja wa Old Trafford kutakuwa na mechi kali ya kibabe kati ya Manchester United dhidi ya Manchester City majira ya saa 1:30 kwa saa za Afrika Mashariki.

Timu hizo msimu huu zimekutana mara tatu ikiwa ni kwenye lingi moja na mechi ya Carabao mara mbili huku United ikishinda mechi mbili na City mechi moja.

Kwenye Ligi Kuu England timu hizo zimekutana mara 45 kutoka mwaka 1992, United imeshinda mechi 22 na City 15 sare zikiwa nane.

Kocha Mkuu wa Manchester City, Pep Guardiola amesema kuwa kwa sasa kuna uwezekano wa kiungo wake Kelvin de Bruyne kuwa sehemu ya kikosi kwa kuwa anaendelea vizuri na kuna uwezekano akaibukia kwenye mechi ya leo.

Kocha wa Manchester United, Ole Gunnar Solksjaer amesema kuwa wana kila sababu ya kushinda kwa kuwa wapo nyumbani.

SOMA NA HII  MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA SPOTIXTRA ALHAMISI