Home Uncategorized YANGA:TUNAWATAMBUA AKINA MKUDE, CHAMA, HATUNA PRESHA

YANGA:TUNAWATAMBUA AKINA MKUDE, CHAMA, HATUNA PRESHA



PAPY Tshishimbi, nahodha wa Yanga amesema kuwa wanatambua aina ya wachezaji wa Simba watakaokutana nao Machi 8, Uwanja wa Taifa hawana presha nao watapambana kupata matokeo.


Yanga itawakaribisha Simba kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara ambao unasubiriwa kwa shauku wakiwa na kumbukumbu ya kulazimisha sare ya kufungana mabao 2-2 kwenye mchezo wa kwanza uliochezwa Januari 4,.

“Tunatambua aina ya wachezaji ambao tunakwenda kukutana nao hako, akina Mkude (Jonas), Chama (Clatous) tunajipanga kuona namna gani tutapata matokeo kwani nasi tuna timu nzuri na bora pia kiushindani.

“Mashabiki wajitokeze kwa wingi kuona namna gani tutapambana ili kupata matokeo chanya,” amesema.

Yanga ikiwa imefunga mabao 29, Tshishimbi ana pasi moja ya bao alilompa Tariq Seif Uwanja wa Taifa kwenye mchezo dhidi ya Biashara United ambapo Yanga ilishinda bao 1-0.
SOMA NA HII  MWAKALEBELA: NINABEBESHWA MIZIGO ISIYONIHUSU