Home Uncategorized BAYERN MUNICH SASA KUANZA KUPIGA MATIZI

BAYERN MUNICH SASA KUANZA KUPIGA MATIZI


KLABU ya Bayern Munich ya Ujerumani wiki hii imetoa taarifa kuwa wachezaji wa klabu hiyo wataanza mazoezi yao rasmi kwa mafungu ili kujikinga na Virusi  vya Corona.

 Awali  Bundesliga ilitarajiwa kurejea Aprili 2, mwaka huu, lakini sasa imesogezwa mpaka Aprili 30 na  hii ni kutokana na ugonjwa wa COVID19 unaosababishwa na Virusi vya Corona kusambaa kwa kasi .
 Bayern inaongoza katika msimamo wa Bundesliga baada ya mechi 25 ikiwa imekusanya jumla ya pointi 55.
 Taarifa  ambayo ilitolewa rasmi na klabu hiyo imeeleza kuwa wachezaji watacheza kwa mafungu ili kujikinga na virusi vya Corona.
“Bayern Munich kikosi cha kwanza wataanza mazoezi wiki hii katika Uwanja wa Sabener Strasse na watakuwa kwenye mafungu ya wachezaji wachache na watafanya kwa zamu ilikuhakikisha wanakuwa sawa.
“ Ili kuzuia maambukizi  tunaomba  mashabiki  wa klabu yetu wasijaribu kusogea katika viwanja vya mazoezi pale ambapo wachezaji watakuwa wakiendelea na majukumu yao kwa usalama wa afya zao na kuzingatia taratibu zote za kujinga  na Virusi vya Corona katika mazingira wanayoishi.
“Bayern wamepata ruhusa hii ya kufanya mazoezi baada ya Chama Cha Soka cha Ujerumani(DFL) kuruhusu kuanza mazoezi kwa tahadhari kuanzia Aprili 5, mwaka huu, lakini mazoezi yatahusisha timu pekee na si watu wengine wa nje.
SOMA NA HII  GAMONDI AWEKA WAZI SIRI YA YANGA KUPATA MATOKEO MAZURI MARA KWA MARA