Home Uncategorized ISHU YA CHAMA, TAMKO LATOLEWA NA SIMBA, YANGA WAJIWEKA KANDO

ISHU YA CHAMA, TAMKO LATOLEWA NA SIMBA, YANGA WAJIWEKA KANDO


UONGOZI wa Simba umesema kuwa hakuna timu itakayomchomoa nyota wao raia wa Zambia kwa sasa, Clatous Chama kutokana na kuhitaji huduma yake.

Kumekuwa na mvutano mkubwa kwa sasa kuhusu Chama kati ya mabosi wa Simba na Yanga ambao wanaelezwa kuiwinda saini yake huku Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela akieleza kuwa wamejiweka pembeni kuhusu suala hilo.

Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema:”Hakuna ambaye anaweza kututisha kwa sasa kuhusu kumpata nyota wetu Chama, tunamhitaji na tunamkataba naye hivyo ikiwa timu inamtaka ni lazima ijipange na ifuate utaratibu tofauti na hapo lazima tutawashtaki,”.

Taarifa ambayo imetolewa kupitia Ukurasa wa Istagram wa Simba imeeleza kuwa Chama amesema kwamba bado ana mkataba na Simba.

Mwakalebela amesema kuwa utaratibu wa usajili anautambua na alifanya hivyo kwa lengo la utani hivyo anaomba msamaha kwa uongozi wa Simba na mashabiki kiujumla.

“Tunajiweka pembeni katika suala hili hii ni kutokana na awali kuwa na mkanganyiko kidogo lakini ilikuwa ni sehemu ya utani, kwa sasa acha maisha yaendelee,” amesema.

SOMA NA HII  WACHEZAJI WAPEWA SOMO HILI LA KUFANYA WAKATI HUU BAADA YA KAMBI KUVUNJWA