Home Uncategorized KIUNGO ALIYEKIPIGA SIMBA NA YANGA AMPA SOMO MWAMNYETO

KIUNGO ALIYEKIPIGA SIMBA NA YANGA AMPA SOMO MWAMNYETO


KIUNGO wa zamani wa Klabu ya Simba na Yanga Athuman Idd Chuji amesema kuwa kwa sasa ndani ya Bongo mchezaji mwenye thamani kwa wazawa ni beki chipukizi wa Coastal Union, Bakari Mwamnyeto.

Chuji anayekipiga kwa sasa ndani ya Singida United amemtaka beki huyo kutulia kabla ya kusaini dili jipya jambo litakalomuongezea thamani.

Mwamnyeto amekuwa kwenye ubora wake msimu huu ambapo safu yake ya ushambuliaji ipo nafasi ya pili kwa timu zilizofungwa mabao machache ikiwa imefungwa mabao 19 baada ya kucheza mechi 28.

Safu ya Simba iliyo chini ya Pascal Wawa inashika nafasi ya kwanza ikiwa imefungwa mabao 15 baada ya kucheza mechi 28.

“Miongoni mwa wachezaji wazawa ambao thamani yao ni kubwa kwa sasa ni Mwamnyeto ambaye anacheza Coastal Union, kwa sasa mambo yamekuwa tofauti na zamani ambapo mambo yalikuwa yanamalizika hata mtaani ila kwa sasa ni lazima mchezaji akae mezani na wale wanaomtaka.

“Muhimu kwa Mwamnyeto ambaye kwa sasa ni miongoni mwa wazawa wenye thamani kutulia kabla ya kupata dili jipya na kutazama maslahi,” amesema.

SOMA NA HII  MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA SPOTIXTRA JUMAPILI