Home Uncategorized KOCHA MKUU WA SIMBA ATOA NENO LAKE KWA MSHAMBULIAJI NAMBA MOJA BONGO

KOCHA MKUU WA SIMBA ATOA NENO LAKE KWA MSHAMBULIAJI NAMBA MOJA BONGO


SVEN Vandenbroeck, Kocha Mkuu wa Simba, amesema amekuwa akishangazwa na uwezo wa mshambuliaji wake, Meddie Kagere ndani ya uwanja kutokana na kufanya kazi bila kuchoka. 

Kagere raia wa Rwanda, ni namba moja kwa utupiaji kwenye Ligi Kuu Bara msimu huu akiwa ametupia mabao 19 na ametoa asisti tano. 

Sven raia wa Ubelgiji, amesema kuwa alianza kumtumia Kagere kwenye mechi yake ya kwanza mbele ya Lipuli ambapo walishinda kwa mabao 4-0, huku mshambuliaji huyo akitupia bao moja.


“Ni mshambuliaji ambaye nimemtumia kwenye mechi nyingi kwa kuwa nilimkuta akiwa fiti na mechi yake ya kwanza alifunga, hili ni jambo ambalo linamaanisha kwamba ni mtu wa kazi kweli ndani ya uwanja, hataki masihara,” alisema Sven.

SOMA NA HII  MASHINE ZINGINE AFCON KUMALIZANA NA YANGA, BOSI ASAFIRI