Home Uncategorized LONGSTAFF AWEKWA KWENYE HESABU ZA AC MILAN ATAJA MASHARTI YA KUWAGA WINO

LONGSTAFF AWEKWA KWENYE HESABU ZA AC MILAN ATAJA MASHARTI YA KUWAGA WINO


MKATABA wa kiungo machachari ndani ya Newcastle United Matty Longstaff unameguka Juni 30 msimu huu huku Klabu ya AC Milan ikiwa sokoni kuisaka saini yake.

Inaripotiwa kuwa tayari kiungo huyo yupo tayari kuongeza kandarasi nyingine iwapo klabu hiyo itakamilisha dili la kupata mmiliki mpya wa klabu hiyo.

Nyota huyo mwenye miaka 20 inaelezwa kuwa yupo tayari kufanya kazi na bosi mpya anayetajwa kuhitaji kuwa mmoja ya wamiliki wa klabu hiyo ambayo ni kampuni kutoka Uarabuni.

Msimu huu nyota huyo amecheza mechi 13 ambapo alianza kwenye mechi 11 amefunga mabao matatu kwenye jumla ya mashindano yote.
SOMA NA HII  REKODI ZAIBEBA SIMBA LEO UWANJA WA TAIFA MBELE YA SINGIDA UNITED