Home Uncategorized HUU HAPA MCHEZO ULIACHA REKODI NYINGI MSIMU HUU NDANI YA LIGI KUU...

HUU HAPA MCHEZO ULIACHA REKODI NYINGI MSIMU HUU NDANI YA LIGI KUU BARA


KWA Msimu wa 2019/20 mpaka unasimishwa kutokana na maambukizi ya Virusi vya Corona mechi ya Simba na Singida United ndiyo iliacha rekodi nyingi 

Miongoni mwa rekodi hizo ni pamoja na:- Meddie Kagere alifunga mabao mengi kwenye mchezo mmoja yalikuwa mabao manne.

Boban mkongwe alipewa kadi nyekundu kwa kosa la kuonekana akimnyoosha Aishi Manula.

Timu ya Singida United haikuwa na dokta kwenye mchezo huo ambapo walikuwa wanasaidiana na madaktari wa Simba.

Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ na Hassan Dilunga walitoa pasi mbilimbili za mabao.

John Bocco alifunga bao lake la nne na alitoa pasi yake ya tatu ya bao.

Ilikuwa mechi ya mwisho kwa Simba na Singida United kwa msimu huu ambapo ile ya mzunguko wa kwanza Simba ilishinda bao 1-0.


Mechi hiyo ilichezwa Uwanja wa Uhuru na Simba ilishinda mabao 8-0.


Ligi ilisimamishwa Machi 17 kutokana na maambukizi ya Virusi vya Corona ambavyo ni janga la dunia.

SOMA NA HII  NAHODHA STARS AFICHUA SIRI YA MAFANIKIO