Home Uncategorized KAGERE AMEKUMBUKA MPIRA, CORONA YAMFANYA ASHINDE NDANI

KAGERE AMEKUMBUKA MPIRA, CORONA YAMFANYA ASHINDE NDANI


MEDDIE Kagere, mshambuliaji namba moja ndani ya Klabu ya Simba amesema kuwa kwa sasa hakuna anachokifanya nchini Rwanda zaidi ya kujifungia ndani kuchukua tahadhari dhidi ya Virusi ya Corona.

Kabla ya Ligi Kuu Tanzania Bara kusimamishwa Machi 17 na Serikali, Kagere alikuwa ametupia mabao 19 na kutoa pasi tano za mabao.

Kagere amesema:”Kwa sasa nipo ndani hakuna ninachokifanya kutokana na kuchukua tahadhari dhidi ya Corona, nimekumbuka kucheza mpira na kufunga ila inashindikana kwa kuwa ligi imesimama.

“Hakuna namna ya kufanya ni lazima tuendelee kuwa watulivu kwa sasa mpaka pale mambo yatakapokuwa sawa.”


SOMA NA HII  MTUPIAJI WA LIPULI HIKI NDICHO ANACHOKIFANYA KWA SASA