Home Uncategorized KIUNGO YANGA AOMBA MKATABA SIMBA

KIUNGO YANGA AOMBA MKATABA SIMBA


KIUNGO wa zamani wa Yanga, Mbrazil, Andrey Coutinho, ameibuka na kuwaambia viongozi wa Simba kuwa yupo tayari kurejea nchini kujiunga na timu hiyo.


Coutinho anayekipiga katika klabu ya Ayutthaya United ya nchini Thailand, aliwahi kuchezea Yanga katika kipindi cha mwaka 2014 hadi 2016, akitokea Taubate SP ya kwao Brazil. 

Coutinho amesema kuwa bado anatamani kuona anapata nafasi nyingine ya kucheza Ligi ya Tanzania akiwa na timu yoyote ikiwemo Simba kama watakuwa tayari kumpa mkataba.


“Sasa hivi nacheza Thailand, lakini bado naikumbuka sana Tanzania kwa sababu ilikuwa nchi yangu ya kwanza kucheza soka la kulipwa, natamani kuona narudi tena kucheza katika timu yoyote, lakini zaidi Simba,” amesema.

SOMA NA HII  MABINGWA WA AFRIKA ALGERIA WANATISHA KINOMA