Home Uncategorized RUVU SHOOTING:TUPO TAYARI KUTOA BURUDANI

RUVU SHOOTING:TUPO TAYARI KUTOA BURUDANI


MASAU Bwire, Ofisa Habari wa Ruvu Shooting amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mechi zao zote 10 zilizobaki kuendelea kutoa burudani kwa mashabiki wao.

Ligi Kuu Tanzania Bara inatarajiwa kuendelea kutimua vumbi Juni 13 ambapo ilisimama tangu Machi 17 kutokana na janga la Virusi vya Corona.

Akizungumza na Saleh Jembe, Bwire amesema kuwa walikosa kuendelea kutoa burudani kwa muda mrefu na kwa sasa wanaamini watwapa mashabiki kile walichokikikosa.

“Kuna mambo ambayo yalitokea hapo nyuma najua kila mmoja anajua ilikuwa ni janga la Corona, kwa kuwa kwa sasa hali imeanza kuwa shwari kwa mujibu wa Serikali tunaamini ni wakati wetu wa kuendelea pale tulipoishia.

“Wachezaji wapo tayari kuendelea kupambana na tuna imani kwamba kazi kubwa itakuwa kwenye kutafuta matokeo hilo lipo kwa wachezaji baada ya kupata maandalizi mazuri,” amesema.

Ruvu Shooting ipo nafasi ya 11 ikiwa imecheza mechi 28 kibindoni ina pointi 39.

SOMA NA HII  KOCHA AFUNGUKA HAYA BAADA YA MANULA KUREJEA KIKOSINI