Home Uncategorized COASTAL UNION: NAMUNGO SIO TIMU NYEPESI,TUPO TAYARI KUPAMBANA

COASTAL UNION: NAMUNGO SIO TIMU NYEPESI,TUPO TAYARI KUPAMBANA

KOCHA Mkuu wa Coastal Union, Juma Mgunda, amesema kuwa kikosi kipo tayari kwa ajili ya mchezo wa ligi dhidi ya Namungo utakaopigwa Uwanja wa Mkwakwani, Tanga, Juni 13.

Mgunda amesema kuwa wachezaji wapo tayari kuendelea na ushindani palepale walipoishia kwa kuwa morali ni kubwa kwa kila mchezaji.

 “Haitakuwa mechi rahisi kwetu kutokana na ushindani uliopo hivyo kikubwa ambacho tunakitazama ni kuona namna gani timu itapata matokeo.

“Mchezo utakuwa mgumu ukizingatia kwamba tulishinda kwenye mchezo wa kwanza tulipocheza nyumbani kwao,” amesema.

Namungo ipo nafasi ya nne kwenye msimamo ikiwa na pointi 50 baada ya kucheza mechi 28 huku Coastal Union ikiwa na pointi ya tano na pointi 46.

SOMA NA HII  MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA CHAMPIONI JUMAMOSI