Home Uncategorized COASTAL UNION WANA JAMBO HILI LEO MKWAKWANI

COASTAL UNION WANA JAMBO HILI LEO MKWAKWANI


COASTAL Union wamesema kuwa watapambana mbele ya wapinzani wao Mtibwa Sugar leo kwenye mchezo wao utakaopigwa majira ya saa 10;00 jioni.

Kocha Mkuu wa Coastal Union, Juma Mgunda amesema kuwa anawatambua vema wapinzani wake na uwezo wao jambo ambalo linamfanya afikiri namna atakavyoweza kuibuka na ushindi.

“Mchezo wetu utakuwa mgumu ukizingatia kwamba tunakutana na timu makini. licha ya hayo tupo tayari kuona kwamba tunapata pointi tatu kwani wachezaji wangu wapo tayari kwa ushindani,” amesema.

Coastal Union ipo nafasi ya tano kwenye msimamo ikiwa na pointi 47 imecheza mechi 29.

SOMA NA HII  STARS YAJIVUNIA UWANJA WA NYUMBANI, SASA KAZI YA BURUNDI KUISHIA TAIFA