Home Uncategorized MBEYA CITY YATOSHANA NGUVU NA TANZANIA PRISONS

MBEYA CITY YATOSHANA NGUVU NA TANZANIA PRISONS


MCHEZO wa kirafiki uliochezwa leo kati ya Mbeya City na Tanzania Prisons umekamilika kwa timu zote kutoshana nguvu.

Mechi hiyo maalumu kwa ajili ya kujipima nguvu imechezwa Uwanja wa Sokoine Mbeya.

Mbeya City iliyo chini ya Amri Said inapambana kurejesha makali ili kuendelea pale ilipoishia kwani ipo kwenye hatari ya kushuka daraja.

Tanzania Prisons iliyo chini ya Adolf Rishard malengo yao ni kumaliza ndani ya tano bora.

SOMA NA HII  DUH SIMBA WANA SIFA, WAPANIA KULETA USHINDANI