Home Uncategorized NAHODHA MKENYA AKUBALI KUTUA SIMBA JUMLAJUMLA

NAHODHA MKENYA AKUBALI KUTUA SIMBA JUMLAJUMLA

MICHAEL Kibagwe, nahodha wa Klabu ya KCB inayoshiriki Ligi Kuu ya Kenya amesema yupo tayari kutua Bongo kuitumikia timu yoyote inayomhitaji kwa sasa.

Beki huyo amekuwa akihusishwa kujiunga na Simba jambo linalofungua njia kwa Mabingwa hao watetezi kupata saini yake kiulaini.

Kwa sasa Simba imekuwa ikihusishwa kusaka saini za mabeki ili kuongeza nguvu kwenye kikosi chao kitaifa na kimataifa.

Kibwage amesema:”Sijafanya mazungumzo na kiongozi yoyote wa Simba mpaka sasa ila wakija mezani na ofa nzuri tutaongea nipo tayari kucheza Bongo. “Napenda kucheza ndani ya Tanzania kwa kuwa kuna mwamko mkubwa Kwenye masuala ya michezo na uwepo wa wadhamini unawafanya wengi wafikiri kuja kucheza Tanzania, “. KCB imemaliza ikiwa nafasi ya tano msimu huu huku Mabingwa wakiwa ni Gor Mahia.

SOMA NA HII  NGUVU YA KIKOSI CHA KMC ZINAHAMIA HUKU KWA SASA, LEO KUANZA MITIZI YA MAANA