Home Uncategorized NAMUNGO:HAITAKUWA RAHISI KUPAMBANA NA COASTAL UNION

NAMUNGO:HAITAKUWA RAHISI KUPAMBANA NA COASTAL UNION


HITIMANA Thiery, Kocha Mkuu wa Klabu ya Namungo amesema kuwa mchezo wao wa kesho dhidi ya Coastal Union utakuwa mgumu ila watapambana kupaa matokeo.

Namungo itashuka uwanja wa Mkwakwani kumenyana na Coastal Union ikiwa na kumbukumbu ya kufungwa mchezo wake wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Majaliwa.

Akizungumza na Saleh Jembe, Thiery amesema kuwa ana imani kwa maandalizi ambayo vijana wake wanayafanya yatawapa matokeo mazuri.

“Sio kazi nyepesi kupambana na Coastal Union, ukizingatia kwamba hatukuwa na mechi za ushindani kwa muda mrefu.

“Licha ya kwamba tumecheza mechi za kirafiki bado haziwezi kutufanya tukawa bora kwa vile ambavyo tumefikiria, ila kwa sasa tunaamini tutapambana na kupata matokeo,” amesema.

SOMA NA HII  KUMBE HATA HUYU HAJASAINI BHANA...