Home Uncategorized YANGA YAFICHUA KILICHO NYUMA YA USHINDI WAO NA MWADUI, ISHU YA MIGOGORO...

YANGA YAFICHUA KILICHO NYUMA YA USHINDI WAO NA MWADUI, ISHU YA MIGOGORO IPO HIVI


JUMA Abdul, nahodha msaidizi wa Yanga amesema kuwa tofauti zao waliziweka kando na kuingia uwanjani kupambana kwa kuwa ni timu moja.

Jana, Juni 14 Yanga ilikuwa na kibarua mbele ya Mwadui FC ambapo ndani ya dakika 90 waliibuka na ushindi wa bao 1-0.

Bao pekee la ushindi lilifungwa na Mapinduzi Balama dakika ya sita akimalizia pasi ya Deus Kaseke.

Kabla ya mchezo huo ilikuwa inaelezwa kuwa kuna mgogoro ndani ya timu jambo ambalo Abdul ameliweka kando.

Nahodha huyo amesema:”Kutoelewana kwa timu hilo suala linazungumzwa tu ila sisi masuala ya migogoro tunaiweka kando huku hesabu zetu ikiwa ni kupambana kupata matokeo mazuri.

“Malengo yetu ni kuona timu inashinda hasa kwenye mechi zetu zote kikubwa ni sapoti ya mashabiki huku wachezaji tukiendelea kutimiza majukumu yetu,” amesema.

Yanga ipo nafasi ya tatu ikiwa na pointi 54 baada ya kucheza mechi 28.

SOMA NA HII  NYOTA HUYU SIMBA ATAJWA KUBEBA MIKOBA YA BOCCO KWENDA POLOKWANE