Home Uncategorized KUMBE CHAMA ISINGEKUWA MPIRA ANGEPIGA MISHE HIZI

KUMBE CHAMA ISINGEKUWA MPIRA ANGEPIGA MISHE HIZI


CLATOUS Chama, kiungo wa Simba amesema kuwa isingekuwa mpira angejihusisha na masuala ya vichekesho kwani ni miongoni mwa vitu ambavyo alikuwa akifikiria kuvifanya wakati anakua.

Chama amekuwa kwenye ubora wake msimu huu kwa upande wa kuichezesha timu ya Simba ambapo akiwa bora ndani ya uwanja Simba huwa katika kasi yake na akipoa timu pia imekuwa ikipoa.

Kibindoni ana jumla ya pasi tisa ndani ya Ligi Kuu Bara na akiwa amefunga mabao mawili pia kwenye ligi.

Ameendelea kuwa kipenzi cha Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck pamoja na mashabiki wa Simba kutokana na juhudi zake ndani ya uwanja.

Chama amesema:”Zama zile wakati ninakua nilikuwa ninafikiria kufanya masuala ya vichekesho kwa kuwa ni vitu ambavyo ninapenda pia ila kwa kuwa nipo kwenye mpira maisha yangu yanaendelea hukuhuku.”

SOMA NA HII  VIDEO: TAZAMA UCHAMBUZI KUHUSU MECHI YA FAINALI YA SIMBA V NAMUNGO