Home Uncategorized MWAKALEBELA AWATAJA WALIOSEMA KUWA ANAIHUJUMU YANGA

MWAKALEBELA AWATAJA WALIOSEMA KUWA ANAIHUJUMU YANGA


FREDRICK Mwakalebela, Makamu Mwenyekiti wa Yanga amesema kuwa waliokuwa wakilalamika kwamba anaihujumu Yanga ni mashabiki wa Yanga ambao walimuona akiwa Iringa bila kujua kwamba alikuwa huko kwa ajili ya matatizo ya kifamilia.

Hivi karibuni sauti ya Mwakalebela ikilalamika kuhusu kudaiwa akiihujumu Yanga ilisambaa jambo lililozua taharuki kwa mashabiki na wadau wa Klabu ya Yanga.

Akizungumza na Saleh Jembe, Mwakalebela amesema kuwa nia ya kusema vile ilikuwa ni kuweka usawa na alikuwa amechoka kulalamikiwa kuwa anaihujumu Yanga jambo ambalo sio la kweli.

“Unajua nilikuwa napata lawama nyingi na kelele nyingi kutoka kwa mashabiki wa Yanga walioniona Iringa wakiamini kwamba ninaihujumu timu, mimi niliumia hasa ukizingatia kwamba ni kweli nilikuwa Iringa lakini nilikuwa kwa ajili ya matatizo ya kifamilia.

“Mama yangu alikuwa anaumwa hivyo nilikuwa huko kwa ajili ya kusimamia masuala ya matibabu, nimerudi Dar naanza kukutana na habari hizo, mashabiki najua kwamba wanaipenda timu lakini wanapaswa waangalie ni namna gani tunaendelea kupambana ili timu iwe bora.

“Michezo yote ambayo nilikuwa na timu tumepata ushindi nakumbuka mchezo wa kwanza dhidi ya Ndanda baada ya Mkwassa kupewa timu tulishinda, nilikwenda na timu Kagera tumeshinda mbele ya Kagera Sugar na hatukupoteza pia mbele ya Biashara United, sasa unaposema naihujumu timu katika lipi?

“Nipo ndani ya Yanga nina uzoefu na masuala ya uongozi nina amini kwamba tutaendelea kufanya mambo mazuri zaidi kwa ajili ya Yanga hivyo mashabiki wazidi kutupa sapoti,” amesema.

 Kesho Yanga inatarajiwa kushuka uwanjani kumenyana na Lipuli FC mchezo wa ligi, Uwanja wa Samora.

SOMA NA HII  ZAHERA AFUNGUKA JUU YA AJIBU KUSAINI SIMBA