Home Uncategorized NIYONZIMA WA YANGA AFUNGUKIA ISHU YA MKATABA WAKE

NIYONZIMA WA YANGA AFUNGUKIA ISHU YA MKATABA WAKE


LICHA ya kubakisha miezi miwili kabla ya mkataba wake kumalizika, kiungo nyota wa Yanga, Haruna Niyonzima, amefunguka kwamba ameamua kuuweka kando mkataba wake mpya na timu hiyo.
Niyonzima amesema ameamua kufanya hivyo kwa kuwa alitaka kwanza wamalize masuala ya ligi kisha aanze mazungumzo na mabosi wake huku akiweka wazi kuwa kama ikishindikana anaweza kuondoka.
Kiungo huyo Mnyarwanda alitua Yanga kipindi cha dirisha dogo Desemba, mwaka jana akitokea AS Kigali ya kwao na kuanguka saini ya miezi sita.
Mnyarwanda huyo amesema kuwa licha ya mkataba wake kwenda kumalizika, lakini kwa sasa ameliweka kando suala.
“Mimi kama mchezaji mkataba wangu unaenda kumalizika hivi karibuni imebaki kama miezi miwili tu lakini siwezi kuzungumzia kwa sasa.

 “Ukiwa mchezaji huwezi kuchagua kambi ila kwa sasa bado siwezi kuzungumzia masuala ya usajili wangu na mkataba wangu ndani ya Yanga,” amesema.
SOMA NA HII  SIMBA YAICHAPA MAJIMAJI MABAO 5-0