Home Uncategorized YANGA YAFANYA MAAMUZI MAGUMU KUHUSU TSHISHIMBI, NIYONZIMA BADO UTATA

YANGA YAFANYA MAAMUZI MAGUMU KUHUSU TSHISHIMBI, NIYONZIMA BADO UTATA


WADHAMINI wa Klabu ya Yanga, Kampuni ya GSM imemuwekea kitita cha Sh milioni 60 kiungo wake mkabaji Mkongomani, Papy Tshishimbi ili aongeze mkataba wa miaka mingine miwili pekee ambazo kama akizikataa, basi rasmi wataachana naye mara baada ya kumalizika kwa msimu huu.
Hiyo ikiwa ni siku chache tangu ziwepo tetesi za nyota huyo kutimka Yanga baada ya kushindwana katika dau la usajili ambalo yeye amelitaka kabla ya wadhamini hao kushindwa kutoa kitita hicho.
Mkongomani huyo ni kati ya wachezaji wanaotarajiwa kumaliza mikataba yao mwishoni mwa msimu huu wengine ni Issa Mohammed ‘Banka’, Jaffary Mohammed, Said Makapu, Juma Abdul, David Molinga na Mrisho Ngassa.
Taarifa zinaeleza kuwa kiungo huyo amekataa kusaini mkataba huo baada ya kutaka Sh 80m badala ya 60m alizowekewa mezani ili asaini mkataba huo.
Mtoa taarifa huyo alisema kuwa mabosi hao wa GSM wamegomea kuongeza dau hilo la usajili huku ukimtaka kwenda kusaini kwenye klabu nyingine itakayomhitaji kama amekataa fedha hizo.
Aliongeza kuwa mabosi wapo kwenye mazungumzo ya mwisho na kiungo wa Rayon Sports ya Rwanda, Ally Niyonzima ambaye anatajwa kuwaniwa na Simba katika kuelekea msimu ujao.
“Upo uwezekano mkubwa wa Yanga kutoendelea na Tshishimbi katika kuelekea msimu ujao, kwani tayari wamempa mkataba muda mrefu inafikia zaidi ya miezi miwili tangu alipopewa ili ausaini.
“Tangu alipopewa mkataba huo, kiungo huyo hajaurudisha mkataba huo aliopewa kwa ajili ya kuusoma, ni baada ya kushindwa kwenye baadhi ya mahitaji yake ikiwemo dau la usajili ambalo yeye aliliomba.
“Aliomba aongezewe Sh 80m ili asaini lakini wadhamini GSM wenyewe wapo tayari kumpa 60m ili asaini mkataba na kama akikataa, basi maamuzi magumu yatafuata ikiwemo kumtafuta kiungo mwingine mkabaji mwenye uwezo mkubwa kama wake atakayekuja kuichezea Yanga,” alisema mtoa taarifa huyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa GSM, Injinia Hersi Said hivi karibuni alisema: “Tulishafanya mazungumzo na Tshishimbi, tupo katika hatua nzuri za kukamilisha usajili na mambo yakienda vizuri atasaini muda wowote.”
Niyonzima naye utata kisa 140m

Wakati huohuo, Ally Niyonzima naye imeelezwa kuwa kinachokwamisha dili lake la kujiunga na Yanga mapema ni maslahi.

Chanzo kutoka Yanga kimeeleza kuwa klabu ilikuwa tayari kutoa Sh 80m na mshahara wa Sh 7m kwa mwezi huku Ally akitaka Sh 140m na mshahara wa Sh 11m kwa mwezi.
“Niyonzima alikuja nchini wiki iliyopita lakini alisharejea kwao, mipango haikukaa sawa na viongozi wa Yanga kwa kuwa alihitaji fedha nyingi ambazo klabu haikuafikia,” alisema mtoa taarifa.
Alipotafutwa Ally juu ya hilo alisema ni kweli walishindwana na viongozi wa Yanga juu ya maslahi binafsi hivyo akaamua aondoke kwa kuwa ana ofa nyingi za timu mbalimbali zinazomhitaji.
SOMA NA HII  SIMBA WAREJEA BONGO KUIWAHI AZAM FC