Home Uncategorized MORRISON WA YANGA AICHUNIA TEAMKIBA NA KUIBUKIA TEAMSAMATTA

MORRISON WA YANGA AICHUNIA TEAMKIBA NA KUIBUKIA TEAMSAMATTA

 

BERNARD Morrison, kiungo mshambuliaji wa Yanga leo amezua jambo lake kwenye mazoezi ya maandalizi ya mchezo wa TeamSamatta na TeamKiba yaliyofanyika Uwanja wa Mkapa, Agosti 7.

Timu za TeamKiba na TeamSamatta kesho zitakutana Uwanja wa Mkapa kucheza mchezo wa hisani wa SamaKiba Foundation ambao hulenga kukusanya mapato na kuzisaidia jamii zenye uhitaji,msimu huu wamepanga kusaidia tena katika suala la elimu.


Ilikuwa namna hii, Morrison jana, Agosti 6 alifanya mazoezi na TeamKiba,kwa kuwa tayari alishatangazwa kuwa atacheza ndani ya kikosi cha TeamKiba ila leo Agosti 7 amewasaliti wenzake wa TeamKiba ambao walikuwa wakifanya mazoezi Uwanja wa Uhuru yeye akaibukia Uwanja wa Taifa na kufanya mazoezi na TeamSamatta.


Alipofika uwanjani aliendelea kufanya mazoezi na wachezaji wenzake chini ya kocha Seleman Matola huku baadhi ya wachezaji aliokuwa nao ikiwa ni pamoja na Erasto Nyonim Mrisho Ngassa, Shomari Kapombe na Juma Kaseja.

Wakati wanaendelea na mazoezi, uongozi wa TeamKiba ulimfuata Matola na kumuomba waondoke na Morrison kwa kuwa timu yake ilikuwa imeanza mazoezi, alichokifanya Morrison ni kutoka nje ya uwanja na kupiga simu kwa mtu ambaye alisema ndiye amemuelekeza aende Uwanja wa Mkapa.


Baada ya mazungumzo hayo, Morrison aliwatazama viongozi wa TeamKiba kisha akarudi uwanjani kuendelea na mazoezi mpaka mwisho.


Akizungumza kuhusu hilo Morrison amesema:”Huu ni mchezo wa hisani hakuna ubaya mimi kuwa TeamSamatta hata kwa Kiba mimi naona ni sawa hakuna tatizo,”.

SOMA NA HII  KIKOSI CHA SIMBA KITAKACHOANZA LEO DHIDI YA NDANDA FC, NANGWANDA