Home Uncategorized SHARAF SHIBOUB ATAJWA KUINGIA ANGA ZA YANGA,NDANI YA SIMBA PANGA LINAMHUSU

SHARAF SHIBOUB ATAJWA KUINGIA ANGA ZA YANGA,NDANI YA SIMBA PANGA LINAMHUSU

 

SHARAF Shiboub,  kiungo wa Simba aliyeibuka ndani ya kikosi hicho akitokea Sudan, shujaa wa mchezo wa ngao ya jamii dhidi ya Azam FC anatajwa kuingia anga za Yanga ambao wanazidi kuimarisha kikosi chao.

Habari zinaeleza kuwa Yanga wanatambua kwamba kiungo huyo hayupo kwenye hesabu za Simba msimu wa 2020/21 hivyo itakuwa rahisi kumpata wao akiwa mchezaji huru.

Mkataba wake wa mwaka mmoja aliosaini ndani ya Simba tayari umekwisha meguka na hajaongezewa mkataba mwingine mpaka anaibukia kwao nchini Sudan.

“Kabla hajaondoka Bongo kuna watu wa Yanga ambao walimfuata Shiboub na kuzungumza naye, waliweka dau mezani ila nyota huyo hakuwaelewa zaidi ya kuwaambia waongeze dau hivyo wanasubiri Simba waachane naye kabisa maana wakisema wawafuate kwa sasa watatajiwa bei ya kukomoa,” ilieleza taarifa hiyo. 

Habari kutoka ndani ya Simba zinaeleza kuwa Shiboub hana nafasi tena ndani ya kikosi hicho licha ya uwezo wake kuwa mkubwa alionyesha jeuri baada ya kurudi wakati ule janga la Virusi vya Corona lilipotulia.

“Shiboub ni mchezaji mzuri lakini ishu ya kuongezewa mkataba Simba itakuwa ngumu, ile likizo ya Corona ilimuongezea kiburi aliporudi alibadilika kidogo tofauti na mwanzo sasa maisha ya jeuri ndani ya Simba hayana nafasi ndio maana unaona hakucheza hata mechi moja, safari inamhusu,” ilieleza taarifahiyo.

Ndani ya Ligi Kuu Bara,  Shiboub ametupia mabao mawili na kutoa jumla ya pasi sita za mabao kati ya 78 yaliyofungwa na timu yake ya Simba.

SOMA NA HII  MASHINE YA KAZI YANGA YATUA LEO BUKOBA NA KUTINGA MAZOEZINI, KESHO KUVAANA NA KAGERA SUGAR