Home Uncategorized KAGERA SUGAR YAJIVUNIA MAJEMBE YA SIMBA NA YANGA

KAGERA SUGAR YAJIVUNIA MAJEMBE YA SIMBA NA YANGA

 


KOCHA Mkuu wa Kagera Sugar, Mecky Maxime amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya msimu mpya wa 2020/21 huku akiamini kwamba usajili uliofanywa utampa matokeo chanya ndani ya ligi.

Kagera Sugar itaanza msimu wa 2020/21 ikiwa na majembe mapya nane ambayo yataanza kazi rasmi Septemba saba kwa kumenyana na JKT Tanzania, Uwanja wa Kaitaba, Bukoba huku wakiwa na maingizo mapya mawili kutoka Simba na Yanga ambao ni beki Ally Mtoni na Mohamed Ibrahim,’Mo Ibra’.

Akizungumza na  Spoti Xtra, Maxime alisema kuwa wamejipanga kwa ajili ya msimu mpya na kila mchezaji anatambua majukumu yake ndani ya uwanja.

“Tumefanya usajili mzuri na tunatambua kwamba msimu utakuwa na ushindani mkubwa ukizingatia kwamba maandalizi yalikuwa mafupi kutokana na janga la Corona, tupo tayari na mashabiki watupe sapoti,” alisema.

Majembe mapya ya kazi yatakayokipiga ndani ya Kagera Sugar ni pamoja na:-Abdalah Mfuko beki kutoka KMC, Ally Nasoro kutoka Mbeya City yeye ni kiungo, Mbaraka Yusuph yeye ni mshambuliaji kutoka Azam FC.

Hassan Mwaterema kutoka JKT Tanzania yeye ni mshambuliaji.Sadat Mohamed akitokea Ruvu Shooting yeye ni winga.Vitalis Mayanga kutoka Ndanda FC yeye ni mshambuliaji.Ally Mtoni kutoka Yanga yeye ni beki na Mohamed Ibrahim, Mo Ibra kutoka Namungo FC alikokuwa kwa mkopo akitokea Klabu ya Simba.

SOMA NA HII  TFF WATOA TAMKO JUU YA OMOG KUINOA TAIFA STARS