Home Uncategorized AZAM FC AKILI ZOTE KWA JKT TANZANIA

AZAM FC AKILI ZOTE KWA JKT TANZANIA

 

UONGOZI wa Azam FC umesema kuwa kupoteza kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar sio mwisho wa mapambano ndani ya Ligi Kuu Bara.


Azam FC chini ya Kocha Mkuu, Aristica Cioaba ilicheza mechi saba mfululizo bila kupoteza na yote ilishinda na kusepa na pointi 21 jumlajumla ikiwa nafasi ya kwanza.


Mchezo wa kwanza ilipoteza kwa kufungwa bao na nyota wa Mtibwa Sugar, Jaffary Kibaya dakika ya 62 kwa guu lake la kushoto akiwa nje ya 18 Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.

Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit amesema kuwa baada ya kupoteza mchezo huo wanajipanga dhidi ya JKT Tanzania. 

“Kupoteza kwetu dhidi ya Mtibwa Sugar sio mbaya ni mwanzo wa kujipanga kwenye mechi zijazo na inatoa tahadhari kwamba tunapaswa kucheza kwa juhudi na kwa mipango zaidi katika kusaka ushindi kwenye mechi zetu.


“Bado ligi inaendelea mapambano yanaendelea, mashabiki watupe sapoti tunaamini kwamba mchezo wetu dhidi ya JKT Tanzania tutafanya vizuri,” amesema.

Mchezo wao dhidi ya JKT Tanzania unatarajiwa kuchezwa Oktoba 30, Uwanja wa Azam Complex.

SOMA NA HII  SIMBA WAANZA KUIVUTIA KASI NAMUNGO FC