Home Uncategorized EVERTON YAIKOMALIA LIVERPOOL NA KUGAWANA POINTI MOJAMOJA KWENYE DABI

EVERTON YAIKOMALIA LIVERPOOL NA KUGAWANA POINTI MOJAMOJA KWENYE DABI


 DABI ya leo Oktoba 17 ndani ya Ligi Kuu England ya Merseyside imekamilika kwa Everton kutoshana nguvu ya kufungana mabao 2-2 na kufanya wagawane pointi mojamoja.

Liverpool ilikuwa ya kwanza kufunga kupitia kwa Sadio Mane aliyepachika bao dakika ya 3 likasawazishwa na Keane wa Everton dakika ya 19.

Mohamed Salah alipachika bao la pili kwa Liverpool dakika ya 72 na kumfanya afikishe jumla ya mabao 100 akiwa na jezi ya Liverpool.

Bao lake lilisawazishwa dakika ya 81 na Calvert Lewin na kuwafanya Liverpool chini ya Jurgen Klopp wasiamini wanachokiona Uwanja wa Goodison Park kwenye ngome ya Carlo Ancelotti wakiwa hawajapoteza mechi msimu huu wakiwa wamecheza tano na kushinda nne huku sare wakipata leo ndani ya Ligi Kuu England.

Everton walimaliza pungufu baada ya mshambuliaji wao Richarlison kuonyeshwa kadi nyekundu dakika ya 90.

SOMA NA HII  MRITHI WA MIKOBA YA JONAS MKUDE NDANI YA SIMBA HUYU HAPA