Home Uncategorized NYOTA WAWILI WA YANGA KUUKOSA MCHEZO WA POLISI TANZANIA

NYOTA WAWILI WA YANGA KUUKOSA MCHEZO WA POLISI TANZANIA




NYOTA wawili wa Yanga wanatarajiwa kuukosa jumla mchezo wa kwanza kwa Kocha Mkuu, Cedric Kaze kutokana na kutokuwa fiti kiafya.  

Ally Makame nyota wa Klabu ya Yanga na Mapinduzi Balama wanatarajiwa kuukosa mchezo wa Ligi Kuu Bara unaotarajiwa kuchezwa Oktoba 22, Uwanja wa Mkapa dhidi ya Polisi Tanzania.

Makame kwa mujibu wa Meneja wa Yanga, Hafidhi Saleh ni kwamba anasumbuliwa na Malaria huku Balama akiendelea kutibu majeraha yake ambayo aliyapata mwishoni mwa msimu uliopita wa 2019/20.

Kwa sasa taryari Balama ameanza mazoezi mepesi ili kujiweka fiti kinachosubiriwa ni ripoti ya dokta kujua kwamba kama anaruhusiwa kuanza kufanya mazoezi na wachezaji wenzake ama la.

Balama msimu uliopita alifunga jumla ya mabao matatu kwenye ligi na bao lake alilomtungua kipa namba moja wa Simba, Aishi Manula liliingia kwenye kinyang’anyiro cha kuwania tuzo ya bao bora kwa msimu wa 2019/20.

Alifunga bao hilo Januari 4, kwenye dabi ambapo dakika 90 zilikamilika kwa timu hizo kutoshana kwa kufungana mabao 2-2, Uwanja wa Mkapa.

Yanga inatarajiwa kumenyana na Polisi Tanzania, Oktoba 22, Uwanja wa Mkapa kwenye mbio za kusaka pointi tatu muhimu. 

Yanga ipo nafasi ya tatu ikiwa na pointi 13 baada ya kucheza mechi tano inakutana na Polisi Tanzania iliyo nafasi ya tano baada ya kucheza mechi sita  ikiwa na pointi 11.

SOMA NA HII  MTIBWA SUGAR: TUNAZITAKA POINTI TATU ZA KAGERA SUGAR