Home Uncategorized MO DEWJI AFUNGUKA KUHUSU MUKOKO TONOMBE, ASEMA MWALIMU KAPELEKA MAPENDEKEZO YA KIUNGO...

MO DEWJI AFUNGUKA KUHUSU MUKOKO TONOMBE, ASEMA MWALIMU KAPELEKA MAPENDEKEZO YA KIUNGO MKABAJI

 



Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Simba, Mohamed Dewji amesema suala la Simba kuwa inamuwania kiungo nyota wa Yanga, Mukoko Tonombe ni propaganda zilizotengenezwa.


Dewji amesema Simba haijawahi kumjadili Mukoko na wala haina habari naye kama inavyoelezwa mitandaoni.



Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Dewji amesema kila suala la usajili wa Simba, ni mapendekezo ya kocha.


“Kocha ndiye anependekeza mchezaji gani anatakiwa, huyo mchezaji hatujawahi kumjadili,” alisema.


Hata hivyo, Dewji alikiri kuwa Kocha Sven van der Broeek amependekeza kusajiliwa kwa kiungi mkabaji kutokana na Gerson Fraga kuwa majeruhi kwa muda mrefu sasa.


Kutokana na hilo, Dewji aliendelea kusisitiza kwamba suala lao la kumsajili kiungi mkabaji litakuwa ni siri.


“Hiyo ni siri, si kwamba tunazihofia timu za hapa ndani. Lakini tunahofia pia hata zile za nje ya Tanzania kwa kuwa kutokana na mwendo mzuri wa Simba, kumekuwa na ushindani mkubwa sana.”


Hivyo karibuni kulizuka taarifa kwamba kutokana na Yanga kuonekana kutaka kumsajili Cleotus Chama kutoka Simba, Msimbazi nao wameamua kuhamishia mashambulizi kwa Mukoko raia wa DRC maarufu kama Ticha.


SOMA NA HII  UKIACHANA NA SOKA, HIKI NI KIPAJI KINGINE CHA DAVID MOLINGA 'FALCAO'