Home Uncategorized NYOTA KMC AOMBA KUSEPA NDANI YA KIKOSI

NYOTA KMC AOMBA KUSEPA NDANI YA KIKOSI


 SALIM Aiyee, nyota wa Klabu ya KMC imeelezwa kuwa ameomba kuondoka ndani ya timu hiyo kutokana na kukosa namba kikosi cha kwanza.

Aiyee aliibukia ndani ya KMC msimu wa 2018/19 akitokea Klabu ya Mwadui FC ambapo alikuwa ni chaguo namba moja ndani ya timu hiyo.

Ila mambo yake yalikuwa magumu msimu wake wa kwanza kwani hakuwa ni chaguo la kwanza ndani ya kikosi hicho na alipopata majeraha basi akajenga ushkaji na nyavu.

Kwa msmu wa 2019/20 alitupia bao moja ndani ya timu yake ilikuwa wakati timu yake ikishinda bao 1-0 dhidi ya Yanga, Uwanja wa Uhuru. 

Msimu huu wa 2020/21 amekwama kufunga ndani ya ligi akiwa ni mshikaji mkubwa wa benchi.

Taarifa kutoka kwa mtu wa karibu wa Aiyee, imeeleza kuwa nyota huyo ameomba kuondoka ndani ya kikosi hicho ambacho kinajenga uwanja wa kisasa pale Mwenge.

“Aiyee ameomba kusepa ndani ya KMC mambo yamekuwa magumu kwake kupenya kikosi cha kwanza,” ilieleza taarifa hiyo.

SOMA NA HII  EXCLUSIVE, YANGA WAIGOMEA VODACOM