Home Uncategorized SITA KUPIGWA PANGA NDANI YA YANGA

SITA KUPIGWA PANGA NDANI YA YANGA

MAKAMU Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Yanga na Mkurugenzi Uwekezaji wa Kampuni ya GSM, Injinia Hersi Said amesema kuwa wapo wachezaji ambao watatolewa kwa mkopo ili kulinda vipaji vyao.

Yanga ikiwa chini ya Kocha Mkuu Cedric Kaze imeendelea kuwa imara kwa kupata matokeo mazuri jambo ambalo limewafanya waendelee kuwa vinara na pointi zao 37.

Injia amesema kuwa wamepokea ripoti kutoka kwa kocha ambayo imetoa maelekezo ya kuwatoa nyota wengine kwa mkopo ili kupata nafasi ya kucheza na kuongeza uwezo.

Miongoni mwa nyota ambao watasepa ndani ya kikosi hicho ni pamoja na Juma Mahadhi huyu tayari ameshapelekwa Ihefu FC, Abdulaziz Makame,Adam Kiondo na Fahad Omar.

Pia inaelezwa kuwa mwingine ambaye huenda akatolewa kwa mkopo ni pamoja na beki Paul Godfrey, mshambuliaji Waziri Junior ambao wamekuwa hawana nafasi kikosi cha kwanza chini ya Cedric Kaze na kufanya idadi ya watakaopigwa panga kuwa sita.


Tayari dirisha dogo limefunguliwa jana Desembe 15 ambapo Yanga imekamilisha usajili wa nyota mmoja ambaye ni Saido Ntibanzokiza, raia wa Burundi akiwa ni mchezaji huru.


Nyota huyo amesaini dili la miaka miwili na jana kwa mara ya kwanza alicheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Singida United na kutupia mabao mawili, wakati Yanga ikishinda mabao 3-0, Uwanja wa Liti, zamani ulikuwa unaitwa Namfua.

SOMA NA HII  UWANJA WA SIMBA WAPIGWA PINI NA TFF