Home Uncategorized WAZAWA WASEPA NA TUZO KWA MARA YA KWANZA

WAZAWA WASEPA NA TUZO KWA MARA YA KWANZA

 


WAZAWA wameweza kuweka rekodi yao kwa msimu wa 2020/21 baada ya kusepa na tuzo zote mbili za mwezi Novemba ndani ya Ligi Kuu Bara.


Tuzo hizo ambazo hutolewa na Kamati ya Tuzo ya Shirikisho la Soka Tanzania ina lengo la kuongeza hamasa na ushindani kwenye ligi ambapo kwa msimu huu wa 2020/21 zilikuwa zimetolewa tuzo mbili na zote zilikwenda kwa wageni.


Ilikuwa ile ya kwanza ya Septemba ambapo ilikwenda kwa mshambuliaji wa Azam FC, Prince Dube raia wa Zimbabwe na ile ya kocha bora alisepa nayo Aristica Cioaba wa Azam FC.


Pia ndani ya mwezi Oktoba ngoma ilikuwa kwa wageni ambapo mchezaji bora alikuwa ni Mukoko Tonombe raia wa Congo anayekipiga ndani ya Yanga na kocha alikuwa ni Cedric Kaze wa Burundi.

Jitihada za wazawa zimeweza kuonekana kwa mwezi Novemba ambapo tuzo zote mbili wamesepa nazo mazima.


Ile ya mchezaji bora imechukuliwa na John Bocco wa Simba na kocha ambaye aliwashinda Abdulrahaman Mussa wa Ruvu Shooting na Deus Kaseke wa Yanga.

Kocha bora ni Charles Mkwasa wa Ruvu Shooting ambaye aliwashinda Mecky Maxime wa Kagera Sugar na Fulgence Novatus wa Gwambina.

SOMA NA HII  WACHEZAJI YANGA WACHELEWESHA KUANZA KWA KAMBI