KOCHA Mkuu wa Yanga, Cedrick Kaze amesema kuwa wanahitaji kulitwaa Kombe la Mapinduzi ili kuongeza hali ya kujiamini kwa wachezaji wake.
Yanga imetinga hatua ya fainali kwa ushindi wa penalti 5-4 dhidi ya Azam FC baada ya dakika 90 kwenye nusu fainali ya kwanza kukamilika kwa timu hizo kufungana bao 1-1.
Bao la Azam FC lilifungwa na Obrey Chirwa na lile la Yanga lilipachikwa kimiani na Tuisila Kisinda.
Kesho Jumatano, Januari 13 zitakutana na Simba kwenye mchezo wa fainali utakaochezwa Uwanja wa Amaan, Visiwani Zanzibar.
Kaze amesema:”Malengo ni kuona kwamba tunatwaa taji la kombe hili ambalo tunashiriki kwa sasa. tunaamini kwamba haitakuwa kazi nyepesi ila tupo tayari kwa ushindani.
“Kikubwa ambacho kipo mashabiki wazidi kutupa sapoti na wachezaji ninajua kwamba watatimiza majukumu yao,” .
Hii inakuwa ni fainali ya pili kwa Yanga kukutana na Simba ambapo ile ya kwanza walikutana msimu wa 2011 na Simba ilishinda mabao 2-1.