Home Simba SC CHAMA, LUIS NA BWALYA WATAJWA KUWA TISHIO KWA MKAPA

CHAMA, LUIS NA BWALYA WATAJWA KUWA TISHIO KWA MKAPA


MCHAMBUZI wa masuala ya michezo ndani ya ardhi ya Bongo, Mwalimu Alex Kashasha amesema kuwa muunganiko wa Clatous Chama, Luis Miquissone na Larry Bwalya ni tishio kwa wapinzani wao ikiwa timu itakuwa kwenye muunganiko imara.


Leo Mei 8, Simba itawakaribisha Yanga kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa majira ya saa 11:00 jioni, Uwanja wa Mkapa.

Kashasha amesema kuwa ili timu ifanye vizuri inahitaji muunganiko pamoja na ushirikiano kuanzia safu ya ulinzi, viungo na ushambuliaji hivyo idara hizi zikifanya kazi kwa ukamilifu wapo wale ambao humalizia muunganiko huo kwa kuamua matokeo hivyo wakipewa nafasi wanaweza kupeleka maumivu kwa wapinzani.

Kashasha amesema kuwa miongoni mwa wachezaji ambao wamekuwa na muunganiko mzuri ndani ya Simba ni pamoja na Bwalya, Luis na Chama.

“Luis na Chama hawa wamehusika kwenye mabao mengi ambayo yamefungwa na Simba yupo na Bwalya huyu naye pia anaufanya muunganiko wao kuwa mkubwa na wenye nguvu.

“Ikiwa watakuwa na muunganiko mzuri kutoka safu ya ushambuliaji mpaka kwenye viungo hapo ndipo ambapo kazi yao imekuwa ikionekana kuwa hatari zaidi.

“Unapozungumzia mpira haumzungumzii mchezaji mmojammoja bali timu kiujumla, lakini kuna wakati mchezaji binafsi huwa na kazi ya kuamua matokeo hasa pale mechi inapokuwa ngumu.

“Hapa unaona mchezaji kama Luis kuna mechi alikuwa anaonekana anaondoka na kijiji cha wachezaji ili kutafuta nafasi, jambo hili nalo ni muhimu kwa wachezaji kujua na kufanya katika kutimiza majukumu yao,” amesema.

Luis na Chama wamehusika kwenye jumla ya mabao 39 ambapo Chama amefunga mabao 7 na kutoa pasi 13 na Luis amefunga mabao 7 na kutoa pasi 9 za mabao wakati Simba ikiwa imefunga mabao 58.


SOMA NA HII  KISA OFA NONO KUTOKA ORLANDO PIRATES... ONYANGO AGOMEA MKATABA MPYA WA SIMBA..ISHU IKO HIVI..