Home Tetesi za usajili BIASHARA UNITED YAWAITA YANGA WAFANYE BIASHARA YA KIPA

BIASHARA UNITED YAWAITA YANGA WAFANYE BIASHARA YA KIPA


 UONGOZI wa Biashara United, umeweka wazi ikiwa mabosi wa Yanga wanahitaji saini ya kipa wao namba moja, Daniel Mgore ni suala la kukaa mezani ili kufanya mazungumzo.


Imekuwa ikielezwa kuwa, Yanga inahitaji kuboresha kikosi chao hasa upande wa mlinda mlango baada ya kipa wao namba moja, Metacha Mnata kusimamishwa kutokana na utovu wa nidhamu, huku mkataba wake ukielekea ukingoni.


Pia katika kikosi hicho, Faroukh Shikalo na Ramadhan Kabwili ambao ndiyo makipa waliobaki, nao mikataba yao inaelekea kumalizika mwishoni mwa msimu huu.

Akizungumza na Spoti Xtra, Mwenyekiti wa Biashara United, Seleman Mataso, alisema kuwa hawana tatizo ikiwa kuna timu inahitaji kumpata kipa wao ni suala la kukaa mezani.


 “Hakuna ambaye anaweza kumzuia mchezaji, huyu Mgore tumemkuza wenyewe kutoka timu ya vijana, kama kuna timu inamuhitaji iwe Yanga ama Azam FC, ni suala la kuzungumza,” .

Kipa huyo alipata nafasi ya kuitwa kwenye timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, msimu uliopita alimaliza ligi akiwa na jumla ya clean sheet 17 na aliingia kwenye kuwania tuzo ya kipa bora iliyokwenda mikononi mwa Aishi Manula.


SOMA NA HII  STAA WA KAGERA SUGAR AZITIA WAZIMU TIMU ZA WAZUNGU ULAYA...BALAA LAKE SIO POA AISEE...